Psalms 86

Kuomba Msaada

Maombi ya Daudi.

1 aEe Bwana, sikia na unijibu,
kwa maana mimi ni maskini na mhitaji.
2 bLinda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako,
wewe ni Mungu wangu,
mwokoe mtumishi wako anayekutumaini.
3 cEe Bwana, nihurumie mimi,
kwa maana ninakuita mchana kutwa.
4 dMpe mtumishi wako furaha,
kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana,
ninainua nafsi yangu.

5 eEe Bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe,
umejaa upendo kwa wote wakuitao.
6 fEe Bwana, sikia maombi yangu,
sikiliza kilio changu unihurumie.
7 gKatika siku ya shida yangu nitakuita,
kwa maana wewe utanijibu.

8 hEe Bwana, katikati ya miungu hakuna kama wewe,
hakuna matendo ya kulinganishwa na yako.
9 iEe Bwana, mataifa yote uliyoyafanya
yatakuja na kuabudu mbele zako;
wataliletea utukufu jina lako.
10 jKwa maana wewe ni mkuu, na unafanya mambo ya ajabu;
wewe peke yako ndiwe Mungu.

11 kEe Bwana, nifundishe njia yako,
nami nitakwenda katika kweli yako;
nipe moyo usiositasita,
ili niweze kulicha jina lako.
12 lEe Bwana wangu, nitakusifu kwa moyo wote;
nitaliadhimisha jina lako milele.
13 mKwa maana upendo wako ni mkuu kwangu;
umeniokoa kutoka kwenye vilindi vya kaburi.
Yaani Kuzimu.


14 oEe Mungu, wenye majivuno wananishambulia;
kundi la watu wakatili linatafuta uhai wangu:
watu wasiokuheshimu wewe.
15 pLakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema,
si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu.
16 qNigeukie na unihurumie;
mpe mtumishi wako nguvu zako,
mwokoe mwana wa mtumishi wako wa kike.
Au: mwokoe mwanao mwaminifu.

17 sNipe ishara ya wema wako,
ili adui zangu waione nao waaibishwe,
kwa kuwa wewe, Ee Bwana,
umenisaidia na kunifariji.
Copyright information for SwhNEN